World Missionary Press

 Njia kwa Mungu - Swahili, Congo

Bookmark and Share  


 

 

 

 

©1992 na Rose Stair Goodman. Sanaa ya jalada, Edwin B. Wallace. Meryl Esemvein, sanaa ya juu na kwa ukurasa 10, 12, 14, 16, 27, 39, 42, 47 na 48. Hakikisha za Biblia zinazotumiwa ni za "La Sainte Bible en Swahili Zaïre, (Congo) Alliance Biblique Universelle", 1989; ila mwisho wa Matayo 6:9-13, Swahili Zanzibar, "The New Testament in Swahili, Union Version", 1985.


 Hakikisha za Biblia zinazotumiwa ni za "La Sainte Bible en Swahili Zaire, (Congo) Alliance Biblique Universelle", 1989; ila mwisho wa Matayo 6:9-13, Swahili Zanzibar, "The New Testament in Swahili, Union Version", 1985.


MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU WETU NA VITU VYOTE VILIVYO HAL — 1 

"Katika mwanzo Mungu aliumba mbigu na dunia." —Mwanzo 1:1

"Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa vilivyo mbinguni na vilivyo duniani...." —Wakolosayi 1:16

"Mubarikwe ninyi na BWANA, aliyefanya mbigu na dunia. Mbingu ni mbingu za BWANA, lakini amewapa wana wa watu inchi." —Zaburi 115:15, 16

Dunia ilikuwa njema wakati Mungu aliimupa mwanadamu. Soma kitabu hiki kidogo kwa kuvumbuwa nini imefanyika.


MUNGU ALITUUMBA — 2

"Mungu akasema: Tufanye mutu kwa mufano wetu, mwenye sura yetu, na watawale...juu ya inchi nzima ....'" —Mwanzo 1:26


MUTU ALIKUWA NAFSI YA UHAI — 3

"BWANA Mungu akafanya mutu wa mavumbi ya inchi, akapuliza pumuzi ya uzima ndani ya pua yake; na mutu alikuwa nafsi* ya uhai." —Mwanzo 2:7

"BWANA Mungu akasema: Si vema mutu awe peke yake; nitamufanyia musaidia....Na BWANA Mungu alileta usingizi muzito kuangukia mutu, akalala; akatwaa mumoja wa mifupa ya mbavu zake, akafunga nyama kwa pahali penyewe; na mufupa wa mbavu BWANA Mungu alioondosha kwa mutu, akafanya mwanamuke, akamupeleka karibu na mutu.'' —Mwanzo 2:18, 21-22

*Nafsi hai maana yake tutakuwa pahali fulani milele.


ADAMU NA HAWA WALIASI MUNGU — 4, 5

Hatungesikiliza Kamwe sauti ya Shetani.

"BWANA Mungu akatwaa mutu, akamutia shambani mwa Edeni kulilima na kulichunga. BWANA Mungu akaagiza mutu akisema: wa kila muti wa shamba unaweza kula; lakini wa muti wa kujua uzuri na ubaya usile kwa maana siku unapokula, hakika utakufa."—Mwanzo 2:15-17 

NYOKA ALIYEITWA VILE DIABOLO AO SHETANI ALIPUUZI MAMLAKA YA MUNGU NAYE AKASEMA UWONGO.

"Nyoka akamwambia mwanamuke: Hakika hamutakufa. Na wakati mwanamuke alipoona ya kama muti ulikuwa muzuri kwa chakula, na ya kama ulipendeza macho, na ya kama ulikuwa muti wa kutamaaniwa akatwaa...akakula; akamupa mume wake vilevile...naye alikula." —Mwanzo 3:4, 6


ADAMU NA HAWA HAWAKUWEZA TENA KUKAA KATIKA SHAMBA — 6

"...BWANA Mungu akamutoa toka shamba la Edeni, alime udongo pale alipotwaliwa....akaweka makerubi...na upanga wa ulimi wa moto...kuchunga nija ya muti wa uzima." —Mwanzo 3:23, 24


ILIKUWA SIKU YA HUZUNI KWA WANADAMU WAKATI ADAMU NA HAWA WALIFANYA ZAMBI — 7

"...Kwa mutu mumoja zambi iliingia ulimwenguni, na kufa kwa nija ya zambi; na hivi kufa kulikuja juu ya watu wote...." —Waroma 5:12

Jambo la kufahamu Kila mutu anazaliwa na hali ya zambi na siku moja atakufa kwa sababu kufa kulikuja kwa njia ya zambi (soma Waroma 5:12 tena).


MUPANGO WA MUNGU KUTUOKOA TOKA ZAMBI ULIKUWA KUTUMA MWANA WAKE WA PEKEE — 8

"Naye atazaa Mwana; nawe utamwita jina lake Yesu, kwa sababu ndiye atakayeokoa watu wake toka zambi zao." —Matayo 1:21

Kwa kukaribia wanadamu, Mwana wa Mungu alipashwa kuja kama Mwana wa mutu. "Maana katika yeye (Yesu Kristo) unakaa utimilifu wote wa Mungu kwa mwili.'' —Wakolosayi 2:9


YESU NI MUNGU ALIYETWAA SURA YA MUTU — 9

"Katika mwanzo alikuwa Neno, na Neno alikuwa pamoja na Mungu, na Neno alikuwa Mungu...Na neno alifanyika mwili, akakaa [akaishi] kwetu...." —Yoane 1:1, 14

"Maneno haya yote yamekuwa ili litimie....Tazama, bikira atachukua mimba, naye atazaa mwana, Nao watamwita jina lake Emanueli; maana yake Mungu pamoja nasi." —Matayo 1:22, 23

"Maana kwa ajili yetu mutoto amezaliwa, tumepewa mutoto mwanamume, na utawala utakuwa juu ya bega lake: Na jina lake litaitwa mwenye ajabu, Mwenye shauri, Mungu Mwenye uwezo, Baba ya milele, Mukubwa wa salama." —Isaya 9:6


YESU KRISTO ZABIHU YETU TAKATIFU — 10

"...Asiyejua zambi...." —2 Wakorinto 5:21 

"Yeye hakutenda zambi...." —1 Petro 2:22

Hakuna zabihu (matoleo) iliyokuwa safi sana ambao mwanadamu angefanya kuondoa zambi.

"Maana haiwezekani kwa damu ya ngombe na mbuzi kuondoa zambi." —Waebrania 10:4

Yesu ni Mwana-kondoo wa Mungu. "Tazama Mwana- Kondoo wa Mungu anayechukua zambi ya ulimwengu."—Yoane 1:29b


YESU ALITOA UZIMA WAKE KUTUOKOA — 11, 12

Yesu alitundikwa ku musalaba wa muti kwa sababu watu wakali walimuchukia. Lakini kufa kwake kulikuwa mupango wa Mungu. Yesu, kwa uhuru wa nia yake yeye mwenyewe, alitoa uzima wake kuokoa wewe na mimi toka zambi zetu.

Yesu akasema: "Hakuna mutu anayeuondoa kwangu [uzima wangu], lakini mimi mwenyewe ninautoa. Nina uwezo kuutoa, na nina uwezo kuutwaa tena...." —Yoane 10:18

TUMEKOMBOLEWA NA DAMU YA MWANA KONDOO WA MUNGU

"...Mumekombolewa [mumenunuliwa], si kwa vitu vinavyoharibika, kwa feza ao zahabu,...lakini kwa damu ya damani, kama ya kondoo asiye na kilema wala alama, damu ya Kristo." —1 Petro 1:18, 19

HAKUNA ZABIHU ZINGINE ZINAZOWEZA KUONDOA ZAMBI

"...Tumepata utakaso (tumefanywa takatifu) kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja." —Waebrania 10:10

"...Tukihesabiwa haki (Tumehesabiwa vema) sasa kwa damu yake,  tutaokolewa katika gazabu kwa yeye."—Waroma 5:9 

"Bwana unikumbuke wakati unapokuja katika ufalme wako."

Mwizi huyu aliamini Yesu na akaokoka. 

"...Kweli ninakuambia, Leo utakuwa pamoja nami katika Paradiso". —Luka 23:43 

Mwizi huyu hakuamini Yesu, basi hakuokoka. 

"...Wakati tulipokuwa tungali wenye zambi [kutotii Mungu], Kristo alikufa kwa ajili yetu." —Waroma 5:8


WOTE WANAOAMINI MWANA WA MUNGU WANA UZIMA — 13

"Kwa maana Mungu alivyopenda ulimwengu, hata kutoa Mwana wake wa pekee, ili kila mutu akimwamini asipotee, lakini apate uzima wa milele." —Yoane 3:16

"Naye alitutoa katika uwezo wa giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa mapendo yake; ndani yake tuna wokovu* wetu, usamehe wa zambi zetu." —Wakolosayi 1:13, 14 

*Wokovu maana yake tumekombolewa.


"AMEFUFUKA!" — 14

"Malaika akajibu, akawaambia wanawake: Mu-

siogope; kwa sababu ninajua ya kama munatafuta Yesu aliyesulibiwa. Yeye si hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Kujeni mwone pahali Bwana alipolala." —Matayo 28:5, 6

 


YESU AMEFUFUKA TOKA WAFU — 15

"Na aliye hai; nami nilikuwa nimekufa, na tazama, mimi ni hai hata milele na milele. Nami nina funguo za mauti, na za Hadeze [Jehanum]." —Ufunuo 1:18

...Kwa sababu mimi ni hai, nanyi mutakuwa hai vilevile." —Yoane 14:19

Kwa sababu Kristo ameshinda kufa, tena ana funguo ya kufa, hatuna haja kuogopa kufa tena.

"Wakati ninapoogopa, nitakutumainia wewe."—Zaburi 56:3                                       (Tazama ukurasa 46 kuhusu ahadi za Mungu.)

YESU ANAWEZA KUKUOKOA NAYE ANAKUOMBEA 

"Lakini yeye, kwa sababu anakaa hata milele...anaweza kuokoa kabisa wao wanaokuja kwake Mungu kwa njia yake; maana yeye ni hai siku zote apate kuwaombea (kuwatetea)." —Waebrania 7:24, 25


WEWE NA MIMI TUNAWEZA KUWA NA UZIMA WA MILELE — 16

Nija gani unachagua? 

Yesu Kristo ni nija ya uzima wa milele pamoja na Mungu. Diabolo (Shetani) ni njia ya kufa kwa milele. Kijama hiki ameamua vema kwa uzima wa milele.

Uzima wa milele Kufa kwa milele

 


CHAGUO GANI UTAKALOFANYA? — 17 

"...Chagueni siku hii ni nani mutakayemutumikia...." —Yosua 24:15 

"...Kwa hivi chagua uzima, upate kuishi, wewe na uzao wako." —Torati 30:19

YESU NI NJIA YA UZIMA WA MILELE

"Wala hakuna wokovu katika mwingine, kwa maana hakuna jina lingine chini ya mbingu waliopewa watu tupate kuokolewa nalo." —Matendo 4:12

"Mimi, mini ni BWANA; na pasipo mimi hapana Mwokozi mwingine." —Isaya 43:11


SABABU GANI TUNAPASHWA KU CHAGUA YESU KAMA — 18
TUNATAKA UZIMA WA MILELE? 

1. Ni Yesu ndiye aliyekuja. 

"...Mimi nimekuja wapate uzima...." —Yoane 10:10 

2. Ni Yesu ndiye aliyetupenda na aliyetukufilia.

"...Mwana wa Mungu aliyenipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu." —Wagalatia 2:20 Yesu alifanyika mutu, mwili na damu sawa tuko, "hata kwa njia ya kufa apate kuharibu yeye aliyekuwa na nguvu za kufa, ndiye Shetani, na kuwafungua wale wote waliokuwa maisha yao yote katika hali ya utumwa, kwa woga wa mauti." —Waebrania 2:14, 15 

3. Damu ya Yesu pekee ni dawa kwa zambi zetu. 

"...Kwa maana ni damu inayofanya upatanisho (usamehe) kwa ajili ya nafsi." —Walawi 17:11 

"...Na damu yake Yesu, Mwana wake, inatusafisha zambi zote." —1 Yoane 1:7 "Ndani yake tuna wokovu wetu, usamehe wa zambi zetu." —Wakolosayi 1:14

4. Ni Kristo ndiye aliyefufuka toka wafu.

"Tukijua ya kuwa Kristo akikwisha kufufuka toka wafu, hakufi tena; wala kufa hakumutawali tena." —Waroma 6:9 

"Tena alikufa kwa ajili ya wote hata walio hai wasiwe hai tena kwa ajili yao wenyewe, lakini kwa ajili yake yeye aliyekufa na kufufuliwa kwa ajili yao." —2 Wakorinto 5:15 

Yesu akasema: "...Kwa sababu mimi ni hai, nanyi mutakuwa hai vilevile." —Yoane 14:19

5. Tunapashwa kuwa na Roho ya Yesu ndani yetu kufufuka kwa uzima milele (Kuishi milele). 

"...Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu." —Wakolosayi 1:27 

"Lakini kama Roho yake yeye aliyefufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyefufua Kristo katika wafu, atawapa uzima kwa miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa sababu ya Roho yake anayekaa ndani yenu." —Waroma 8:11 

UWE NA HAKIKA ROHO WA YESU ANAKAA NDANI YAKO "               ...Lakini kama mutu ye yote asipokuwa na Roho ya Kristo huyu si mutu wake." —Waroma 8:9


NAMNA GANI UNAWEZA PATA UZIMA WA MILELE — 22

Fuata mwongozo kuanza ukurasa 24.

"Hata mutoto anajijulisha kwa njia ya matendo yake ...."       —Mezali 20:11

"Yesu ananipenda, ninajua, Biblia inaniambia hivi."


 YESU ANAPENDA WATOTO WOTE — 23 

"Lakini Yesu akawaita kwake, akisema: Mwache watoto wadogo waje kwangu; musiwakataze, sababu ufalme wa Mungu ni kwao wa namna hii." —Luka 18:16

"Vivyo hivyo haipendezi Baba yenu aliye mbinguni mumoja wa wadogo hawa apotee [aharibiwe ao apotee milele]." —Matayo 18:14

Haizuru uwe nani ao wapi unapoishi, Yesu anakupenda alikufa kwa ajili yako. Yesu anataka mapendo yako vilevile. Unaweza kuonyesha mapendo yako kwa Yesu kwa njia ya kumutii.

"Kama mukinipenda, mutatii amri zangu." —Yoane 14:15


NAMNA YA KUPATA NJIA YAKO KWA MUNGU — 24 - 28

1. Kubali wewe ni mwenye zambi [umemuasi Mungu].

"Kwa sababu wote wamefanya zambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu." —Waroma 3:23

2. Kuja kwa Mungu kupitia Yesu Kristo.

"Kwa sababu Mungu ni mumoja tu na mupatanishi katikati ya Mungu na watu ni mumoja, yule mutu Kristo Yesu." —1 Timoteo 2:5

"Naye [Yesu], kwa sababu hii anaweza kuokoa kabisa wao wanaokuja kwake Mungu kwa njia yake...." —Waebrania 7:25 

Yesu akasema: "...Naye anayekuja kwangu sitamutupa inje kabisa." —Yoane 6:37

3. Tubu zambi zako.
(Kutubu maana yake kujuta sana ku acha zambi.)

"Tubuni basi, mugeuke, ili zambi zenu ziondoshwe...." —Matendo 3:19 

"Bwana...ni muvumilivu kwenu asiyetaka mutu mumoja kupotea, lakini wote wafike kutubu." —2 Petro 3:9 

4. Kiri zambi zako kwa Yesu. (Kukiri maana yake kusema kwa kinywa ao kujitambua.) 

"Tukikiri zambi zetu yeye ni mwa- minifu na wa haki hata atu- ondolee za- mbi zetu...." —1 Yoane 1:9

Juu ya mistari ifuatayo, andika na herufi dogo ao kubwa shairi la 1 Yoane 1:9 lililopatikana kwa mukono wa maombi katika ukurasa 25.

______________________________________________
______________________________________________
______________________________________________
______________________________________________

5. Acha zambi zako.

(Kuacha ina maana ya kukataa ao kukomesha.)

"Yeye anayefunika makosa yake hatasitawi: Lakini yeye anayeyakiri na kuyaacha atapata rehema." —Mezali 28:13

"Acha uovu, na tenda mema...." —Zaburi 37:27

"Kwa maana mumeokolewa kwa neema kwa njia ya imani,...ni zawadi ya Mungu, si kwa matendo, asiwe mutu atakayejisifu." —Waefeso 2:8, 9 

6. Amini Yesu Kristo. 

"...Kama ukikiri kwa kinywa chako ya kuwa Yesu ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimufufua toka wafu, utaokolewa." —Waroma 10:9

"...Amini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokolewa pamoja na nyumba yako." —Matendo 16:31

 7. Pokea Yesu Kristo moyoni na maishani mwako. 

Unaweza tu kufungua mulango wa moyo wako na kua- lika Yesu kuingia. Yesu akasema: "Tazama, ninasimama kwa mulango, ninapiga hodi; kama mutu akisikia sauti yangu na kufungua mulango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami." —Ufunuo 3:20

"Lakini wote waliomupokea aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu, ndio wale walioamini jina lake." —Yoane 1:12


MWONGOZO WA MAOMBI — 29 

Kama haujaomba mbele na unahitaji musaada kwa kuomba, unaweza kufuata maombi haya kama mwongozi: 

Bwana Yesu mupenzi, Asante kwa kifo chako musalabani kuondoa zambi zangu. Ninasikitika kwa mambo yote mabaya niliyoyafanya. Tafazali ninakualika kuingia na kukaa moyoni mwangu milele. Ninakuamini kweli sasa kusaficha moyo wangu. Ninakupokea kuwa Bwana na Mwokozi wangu wa pekee. Katika jina la Yesu, Amina.


PAMOJA NA YESU MOYONI MWAKO UNA UZIMA WA MILELE — 30

"...Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu ni katika Mwana wake. Yeye aliye na Mwana ni mwenye uzima...." —1 Yoane 5:11, 12 

"...Yeye anayesikia neno langu na kumwamini yeye aliyenituma ...amepita kutoka mauti kuingia uzima."—Yoane 5:24 

Na wakati mwili wako unakufa, uko pamoja na Bwana (2 Wakorinto 5:8). "...Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu." —Wakolosayi 1:27 

Kama umeuliza Yesu kusamehe zambi zako, na kuamini Bwana Yesu Kristo kuwa Mwokozi wako, andika jina lako chini:


NAMNA YA KUENDELEA KUFWATA YESU — 31 

Soma mashairi katika Biblia (Neno la Mungu) siku zote na uyashike moyoni mwako kwa njia ya kujifunza kwa ufahamu mashairi muhimu ambao yamekusaidia. (Mengi ni ndani ya kitabu hiki kidogo.) "Kila andiko limepewa kwa maongozi ya Mungu, na linafaa kwa mafundisho, na kwa kuonya watu juu ya makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa mafundisho katika haki." —2 Timoteo 3:16


ZUNGUMUZA NA YESU KILA SIKU KWA MAOMBI — 32

Shukuru Yesu, kwa mambo yote mazuri katika maisha. Umusifu kwa vitu vyote alivyokutendea na kwa kuokoa nafsi yako. Omba kwa kila hitaji unalo. Omba katika jina la Yesu. "...Kama tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, anatusikia."—1 Yoane 5:14 

"...Kila neno munaloomba Baba kwa jina langu, atawapa ninyi."—Yoane 16:23

"...Na kuombeana...." —Yakobo 5:16a  

"...Ombee wenye kuwazarau, na kuwatesa ninyi." —Matayo 5:44


MAOMBI AMBAO YESU ALIFUNDISHA WANAFUNZI WAKE — 33

(Mwanafunzi ni mutu anayefuata Yesu.)

Yesu akawaambia wanafunzi wake kuomba hivi:

"Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama mbinguni. Utupe sisi leo chakula chetu cha kila siku. Utusamehe deni zetu, Kama sisi vilevile tunavyosamehe wadeni wetu. Na usitulete katika majaribu, lakini utuokoe na yule mwovu (kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu hata milele. Amina.)" —Matayo 6:9-13

Maombi haya yangalijifunzwa kwa ufahamu. Waamini wanaombaka maombi haya pamoja kwa sauti.


AMRI KUMI ZA MUNGU ZINATUFUNDISHA NAMNA YA KUISHI — 34, 35
(Kutoka, sura 20) 

Ine za kwanza ni kuhusu mapendo yetu kwa Mungu 

1. "Usiwe na miungu mingine ila mimi."                                                                       

2. "Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala wa kitu kilicho mbinguni juu, wala duniani...usijiiname mbele yao kuzitumikia."                                                                

3. "Usitaje jina la Mungu wako bule."                                                                          

4. "Kumbuka siku ya sabato uitakase." 

Sita za mwisho ni kuhusu mapendo yetu kwa watu

AMRI 10 (zinaendelea) 

5. "Heshimu baba yako na mama yako."

6. "Usiue."

7. "Usizini" (Uzini ni kulalana kwa kukosa unaminifu wa bwana ao muke.)

8. "Usiibe."

9. "Usishuhudie jirani yako uwongo."

10. "Usitamani nyumba ya jirani yako...."

KUTII MUNGU KUNALETA JIBU KWA MAOMBI YETU

"Na lo lote tunaloomba, tunalipokea kwake, kwa kuwa tu nashika amri zake, na kutenda maneno yanayopendeza machoni mwake." —1 Yoane 3:22


AMRI MBILI KUBWA ZAIDI — 36

Mapendo kwa Mungu 

1. "Yesu akamwambia: Upende Bwana Mungu wako na moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ni amri iliyo kubwa na ya kwanza."         —Matayo 22:37, 38 

Mapendo kwa Watu 

2. "Na ya pili inafanana nayo ni hii: Penda jirani yako kama wewe mwenyewe." —Matayo 22:39 

Amri kumi zote (ukurasa 34 na 35) zinaingia ndani ya amri 2 kubwa zaidi.

M A P E N D O


MAPENDO NI MAKUBWA KULIKO YOTE — 37, 38
"Sura Kubwa Ya Mapendo" 
(1 Wakorinto 13:1-8, 13) 

1Kama nikisema na lugha za watu na za malaika, lakini sina mapendo, nimekuwa kama shaba inayolia, ao upatu wa kuvuma. 2Na kama ikiwa nina unabii, na kufahamu siri zote na maarifa yote; na kama ikiwa nina imani yote, hata niweze kuhamisha milima, kama sina mapendo, mimi si kitu. 3Na kama nikatoa (nikawapa) mali zangu zote kulisha masikini, tena nikitoa mwili wangu niungue kwa moto, lakini sina mapendo, hainiletei mimi faida. 4Mapendo yanavumilia, ni upole; mapendo hayajui wivu, mapendo hayajisifu; hayajivuni, 5Hayakosi kuwa na adabu, hayatafuti maneno yake, hayakasiriki mbio, hayahe- sabu mabaya; 6Hayafurahi kwa uzalimu [makosa], lakini yanafurahi pamoja na kweli: 7Yanahimili maneno yote, yanaamini maneno yote, yanatumaini maneno yote, yanavumilia maneno yote. 8Mapendo hayapunguki hata kidogo: lakini kama ukiwa unabii, utaondoshwa; kama zikiwa lugha, zitakoma, kama yakiwa maarifa, yataondoshwa. 13Basi, sasa inadumu imani, tumaini, mapendo, hizi tatu; lakini neno kubwa katikati ya maneno haya ni mapendo. 

MUNGU NIMAPENDO

"...Mungu ni mapendo, naye anayekaa katika mapendo, anakaa ndani ya Mungu na Mungu anakaa ndani yake." —1 Yoane 4:16


YESU ANAKUHITAJI KUSHUHUDIA WENGINE — 39

(nyumbani, chuoni, kanisani, pahaili pote)

Yesu akasema: Kwenda kwa nyumba yako kwa watu wako kuwaambia maneno makubwa gani Bwana aliyofanya juu yako na namna alivyokurehemu. Marko 5:19

 


NAMNA YA KUJUA MUTOTO WA KWELI WA MUNGU — 40, 41

"Kwa hivi mutawatambua kwa njia ya matunda yao." —Matayo 7:20 

"Lakini matunda ya Roho ni mapendo, furaha, salama, uvumili- vu, neema, wema, uaminifu, upole, ujizuiza....—Wagalatia 5:22, 23 

MUTOTO WA KWELI WA MUNGU ANASAMEHE WENGINE

"Kwa sababu kama ninyi munasamehe watu makosa [mabaya] yao, Baba yenu ya mbinguni atawasamehe ninyi vilevile." —Matayo 6:14 

MANENO 7 MUNGU ANAYOYACHUKIA 

"Macho ya kiburi, ulimi wa kusema uwongo, na mikono inayomwanga damu isiyo na kosa, na moyo unaowaza mawazo mabaya, miguu iliyo mepesi kukimbilia uovu, mushuhuda wa uwongo anayesema uwongo, naye anayepanda mbegu ya fitina kati ya ndugu." —Mezali 6:17-19

MATENDO YA MWILI: 

"...Uasherati, uzini [kulalana kati ya watu wasiyeoa bado],... kuabudu sanamu, ulozi, uadui,... husuda, uuaji wa mutu, ulevi,...na yanayofanana na maneno haya;... watu wale wanaotenda maneno ya namna hii, hawatariti ufalme wa Mungu." —Wagalatia 5:19-21

 "...Wala wakike...wala wizi, wala wenye tamaa...." —1 Wakorinto 6:9-10

RUHUSU YESU AKUJAZE ROHO YAKE NA AKUTAKASE 

"Na wengine kwenu mulikuwa hivi; lakini mulioshwa, lakini mulitakaswa [mulifanywa takatifu]...katika jina la Bwana Yesu, na katika Roho ya Mungu wetu." —1 Wakorinto 6:11


HAKIKA YA UWEPO WA MOTO — 42

(Roma Luka 16:19-26.)

Uwe na hakika unaamini Yesu Kristo. Ataandika jina lako katika kitabu chake cha uzima.

"Na ikiwa mutu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto." —Ufunuo 20:15


YESU NDIYE NJIA PEKEE KWA MUNGU — 43 

"...Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu ni katika Mwana wake." —1 Yoane 5:11

"Kwa maana mushahara wa zambi ni mauti, lakini zawadi ya Mungu ni uzima wa milele katika Yesu Kristo Bwana yetu." —Waroma 6:23

"Anayeamini Mwana ana uzima wa milele; na asiyetii Mwana hataona uzima, lakini gazabu ya Mungu inakaa juu yake." —Yoane 3:36

"Yesu akamwambia: Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima: mutu hakuji kwa Baba, ila kwa mimi." —Yoane 14:6


HAKIKA YA UWEPO WA MBINGU — 44

Ndani ya maono ya Yoane katika Ufunuo 21 aliona mbingu mupya na dunia mupya. Naye atapangusa kila chozi katika macho yao; wala mauti haitakuwa tena; wala maombolezo, wala kilio, wala uchungu hautakuwa tena; kwa maana maneno ya kwanza yamekwisha kupita. Na yeye anayeketi juu ya kiti cha ufalme akasema: Tazama, ninafanya yote kuwa mapya.... —Ufunuo 21:4, 5 

Yoane aliona vile Muji takatifu, Yerusalem mupya, ukishuka toka kwa Mungu mbinguni. "...Na muji ule ulikuwa wa zahabu safi, mufano wa kioo safi. Na misingi ya ukuta wa muji ilikuwa imepambwa kwa mawe ya bei ya damani ya kila namna ...." —Ufunuo 21:18, 19


YESU AMEKWENDA KUTENGENEZA NYUMBA KWA WOTE WANAOMWAMINI — 45

Musifazaike mioyoni mwenu: munaamini Mungu, muniamini mimi vilevile. Katika nyumba ya Baba yangu ni makao mengi; kama sivyo ningaliwaambia ninyi; ninakwenda kuwatengenezea ninyi pahali. Na kama ninakwenda kuwatengenezea ninyi pahali, nitakuja tena, na nitawakaribisha ninyi kwangu; pahali ninapokaa mimi, mukae vilevile. —Yoane 14:1-3 

TANGAZA HABARI NJEMA HII KWA WENGINE 

Yesu akasema, Kwendeni katika dunia pia, mukahubiri Habari Njema kwa kila mutu." —Marko 16:15

 "...Naye anayevuta roho za watu ni mwenye hekima." —Mezali 11:30


AHADI ZA MUNGU KWA WATOTO WAKE — 46

"...Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha hata kidogo." —Waebrania 13:5

"Maana ataagiza malaika yake juu yako, wakuchunge katika nija zako zote."          —Zaburi 91:11

"...Hakuna mutu anayeweza kuwanyanganya toka mukono wa Baba yangu." —Yoane 10:29

"...Mimi ni pamoja nanyi siku zote hata mwisho wa dunia." —Matayo 28:20

"Usiogope maneno yote yatakayokupata....Uwe mwaminifu mupaka kufa, nami nitakupa taji ya uzima." —Ufunuo 2:10

"Uniite, nami nitakujibu...." —Yeremia 33:3


YESU ANAKUJA TENA — 47 

Kila mutu atafufuka toka wafu. "...Saa itakuja na watu wote walio katika makaburi watasikia sauti yake, nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuko wa uzima, na wale waliofanya mabaya, kwa ufufuko wa hukumu." —Yoane 5:28, 29

Wafu katika Kristo watafufuka kwanza.

"Kisha sisi tulio hai, tuliobaki, tutanyanyuliwa pamoja nao katika mawingu, kukutana na Bwana katika hewa, na hivi tutakuwa pamoja na Bwana milele." —1 Watesalonika 4:17

"...Tazameni, ombeni, maana hamujui wakati ule." —Marko 13:33


YESU ATAKUJA JE? — 48

"Tazama anakuja na mawingu; na kila jicho litamwona...." —Ufunuo 1:7 

Angalisho kwa wapinga Kristo na manabii ya uwongo. 

"...Wakati mutu atakapowaambia ninyi: Tazama, Kristo ni hapa, ao kule; musiamini. Basi kama wakiwaambia ninyi: Tazama, yeye ni jangwani; musitoke; Tazama, yeye ni katika vyumba vya ndani nyumbani, musisadiki."—Matayo 24:23, 26 

YESU ATAKUJA UPESI KATIKA MAWINGU YA MBINGU

"Kwa maana kama umeme unavyokuja toka mashariki na unaonekana hata mangaribi; hivi kuja kwa Mwana wa watu kutakavyokuwa vile. ...Na mataifa yote ya dunia...wataoma Mwana wa watu akikuja katika mawingu ya mbingu pamoja na uwezo na utukufu...." —Matayo 24:27, 30


ZABURI YA MUCHUNGAJI

(Zaburi 23)

1BWANA ni muchungaji wangu; sitapungukiwa na kitu. 2Ananilalisha katika malisho ya majani mabichi; ananiongoza kando ya maji matulivu. 3Anarudisha nafsi yangu; ananiongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.

4Ndiyo, hata nikipita kati ya bonde la kivuli cha mauti, sitaogopa mabaya; kwa maana wewe ni pamoja nami; gongo lako na fimbo yako zinanifariji. 5Unanitengenezea meza mbele ya adui zangu; umenipakalia mafuta kichwani; kikombe changu kinafurika.

6Hakika wema na rehema zitanifuata siku zote za maisha yangu; na nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.


If you are interested in receiving additional Scripture booklets, write to the publisher in English at the address below or order online:

World Missionary Press, Inc. 
P.O. Box 120 
New Paris, Indiana 46553-0120 U.S.A.

This version of Swahili is called Swahili Congo. It was formerly known as Zaire Swahili. 


               World Missionary Press Home Page | Go to the Top of This Page

Hit Counter